Ofisa mtendaji wa kijiji cha Naitoria wilayani Monduli jijini Arusha, Faraji Shaban ambaye taarifa zake zimesambaa katika mitandao juu ya kumfumania mkewe amesema ameamua kumuachia Mungu suala hilo.
Akizungumza na Mwananchi leo, Shaban amesema ingawa mkewe Amina Agustino ametoroka nyumbani tangu juzi usiku baada ya tukio hilo, lakini ameamua kurejea hospitali Dodoma kupata matibabu ya Figo.
"Ni kweli nilipata taarifa za mke wangu kunisaliti nikiwa katika matibabu, nikarudi usiku na kuandaa mtego ndipo niliwakuta ndani kwangu eneo la Kigongoni Monduli na Faraja mkazi wa Kijenge Arusha," amesema.
Amesema aliripoti tukio hilo polisi na mtuhumiwa alikamatwa na kwamba taratibu zinaendelea za kipolisi.
Hata hivyo, amesema hakusudii kuendelea na kesi hiyo kwani haina faida kwenye maisha yake.
"Mimi mke kitaratibu nimemuacha na Mungu atakwenda kuwahukumu wote," amesema.
Amesema mkewe Amina alifanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja .
Ofisa mmoja wa jeshi la polisi wilaya ya Monduli alikiri kufunguliwa taarifa za tukio hilo na uchunguzi unaendelea.
Social Plugin