Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LAWRENCE MASHA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI MTENDAJI WA FASTJET TANZANIA

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha ameteuliwa kuwa mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya usafiri wa anga, Fastjet.


Taarifa ya kampuni hiyo inasema Masha atashirikiana kwa ukaribu na meneja mkuu wa Fastjet, Derrick Luembe pamoja na menejimenti kunyoosha operesheni zake nchini.


Jukumu jingine atakalolisimamia kwa ukaribu ni mpango wa Fastjet Tanzania kujitegemea kutoka Fastjet PLC yenye makao makuu yake nchini Uingereza.


“Kwa uzoefu alionao, bodi inaamini atakuwa na mchango mkubwa kwenye kampuni hii,” inasema taarifa hiyo.


Mbali na kuteuliwa kushika wadhifa huo wa juu ndani ya Fastjet, Masha pia ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Kiwanda cha Saruji cha Tanga na Ecoprotection Limited na mjumbe wa bodi ya kampuni ya Newforest na mshirika mtendaji wa kampuni ya uwakili ya Gabriel and Co.


Fastjet ilifungua ofisi zake nchini mwaka 2012 kisha kuanza kutoa huduma za usafiri kwenda mikoa ya Kilimanjaro na Mwanza. Baadaye ilijitanua kwa kuwa na ofisi jijini Nairobi (Kenya), Accra (Ghana) na Luanda (Angola).


Masha aliwahi kuwa mbunge wa Nyamagama kati ya mwaka 2005 hadi 2010 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla baadaye hajatimkia Chadema alikodumu kwa miaka miwili na kurejea tena CCM.


Masha amewahi kuwa naibu waziri wa nishati na madini, waziri wa mambo ya ndani na mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Oxygen.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com