Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Msataafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili katika eneo la Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
***
***
Rais John Magufuli amewasili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tayari kwa uzinduzi wa maktaba ya kisasa iliyojengwa na serikali ya China.
Rais Magufuli amewasili katika viwanja vya chuo Saa 9:40 asubuhi leo Jumanne Novemba 27, 2018 na kuanza kukagua maktaba hiyo kabla ya kuungana na watu mbalimbali waliohudhuria katika ufunguzi huo.
Maktaba hiyo inayozinduliwa leo ina uwezo wa kuhudumia wasomaji 2,100 kwa wakati mmoja huku ikiwa na uwezo wa kutunza vitabu 400,000.
Mbali na hilo, pia maktaba hiyo ina ukumbi wa mikutano ulio na uwezo wa kuchukua watu 600.
Viongozi mbalimbali wamehudhuria hafla hiyo.
Miongoni mwao ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa baraza la UDSM, Jaji mstaafu Damiani Lubuva, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo, Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Pia, wapo Jaji mstaafu Joseph Warioba, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro
Na Aurea Simtowe, Mwananchi
Social Plugin