Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KANGI LUGOLA AAGIZA VIGOGO WA POLISI KIGOMA KUTUMBULIWA SAKATA LILILOMPELEKA ZITTO POLISI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania, (IGP) Simon Sirro kuwaondoa katika nafasi zao Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma na mkuu wa operesheni mkoa huo. 

Ameyasema hayo akiwa katika ziara yake wilayani Uvinza mkoani humo leo Jumapili Novemba 11, 2018, ambapo zilitokea vurugu baina ya polisi na wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na kusababisha vifo.

Waziri huyo pia ameagiza kuondolewa kwa mkuu wa intelijensia wa wilaya ya Uvinza, mkuu wa polisi wa wilaya pamoja na kuwahamisha vituo askari wote wa kituo cha Polisi cha Mpeta na Nguruka. 

Mwishoni mwa Oktoba kuliliripotiwa mapigano katika wilaya hiyo ambayo chanzo chake kilielezwa ni mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.

Kiongozi wa chama cha ACT- wazalendo, Zitto Kabwe alizungumzia mauaji hayo katika mkutano wake na wanahabari, Oktoba 29 ambapo alipingana na taarifa ya Jeshi la Polisi juu ya vifo vilivyotokea katika mapigano hayo, akidai vifo vingi zaidi vimetokea, hali iliyopelekea kuitwa kituo cha polisi kwaajili ya mahojiano.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com