WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amezitaka familia za askari kutozitamani posho za chakula, badala yake watumie mishahara ya askari hao.
Lugola ametoa agizo hilo leo tarehe 14 Novemba 2018 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.
“Kweli askari wanapokwenda mafunzoni fedha zao za chakula huwafata kokote wanakokwenda, lengo la fedha kwa ajili ya lishe tunaaka jeshi lenye lishe fedha hizi lazima azitumie kama fedha za chakula.
“Natoa wito wa familia za polisi kuna wakati wanazitamani wanazikodolea macho ninaomba waziache posho hizi watumie mishahara, posho wawaachie wenyewe,” amesema Lugola.
Aidha, Lugola amesema serikali itaendelea kuhuisha posho mablimbali za askari ili ziweze kuwanufaisha.
Social Plugin