Mamlaka ya Uhamiaji nchini, imesema imeanzisha zoezi maalum la utambuzi wa abiria watakaokuwa wakisafiri kwa kutumia vitambulisho vya taifa kwa baadhi ya wasafiri wa mikoa minne nchini, lengo likiwa ni kuimarisha suala la ulinzi na usalama.
Miongoni mwa mikoa ambayo zoezi hilo limeanza ni mkoa wa Dodoma, Kagera, Kigoma, pamoja na mkoa wa Mara ambapo kwa abiria ambao watakuwa hawana vitambulisho watalazimika kutoa maelezo ya ziada ili kupata hati ya mabasi ya kusafiria.
Akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda amesema “tumegundua kuwa wahamiaji haramu wamekuja na mbinu mpya ya kusafiri kwa kutumia mabasi na kupenyeza kuingia nchini na kuishi kinyume cha utaratibu, tutaanza kutumia vitambulisho vya taifa na kura kukata tiketi.”
“Tutafanya majaribio kwa muda mfupi ili kujifunza changamoto zikoje kabla ya kutangaza agizo la nchi nzima kwa hiyo tunaenda awamu kwa awamu, kwa maeneo ambayo hawana vitambulisho wajitahidi kuwasiliana na mamlaka husika ili kupata vitambulisho.”
Kuhusiana na wasafiri binafsi “tumeona kwanza kwa tuanze kwa wasafirishaji wakubwa ndiyo tuanze nao kwa kuwa wamekuwa wakutumia mbinu mpya, lazima tuulizeni, tunapokuwa kwenye basi ili tufahamiane wenyewe kwa wenyewe”, ameongeza Mtanda.
Kama hutokuwa na vitambulisho vyote hivyo ambavyo vimeorodheshwa basi hutoweza kusafiri. vitambulisho vinavyohitajika ni pamoja na; Uraia, Leseni ya udereva, kitambulisho cha Mpiga kura na Hati ya kusafiria na kwa wanafunzi watatumia vitambulisho vya shule.
Chanzo- EATV
Social Plugin