Hayo yamebainika leo Jumatatu Novemba 26, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi.
Kesi ya Zitto iko mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi na imepangwa usikilizwaji wa awali Desemba 13 mwaka huu.
Inadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya ofisi ya chama cha ACT Wazalendo mshtakiwa akiwa katika mkutano huo kwa nia ya kuleta chuki kwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la polisi alitoa Maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.
Katika shtaka la pili, Kweka alidai kuwa siku na mahali hapo, Zitto Kijitonyama alitoa Maneno ya uchochezi ambayo yalikuwa na lengo lenye kuleta hofu.
Aidha Zitto anadaiwa Kutoa waraka kwa umma ukiwa na Maneno ya kichochezi kwa nia ya kuleta chuki kwa Watanzania dhidi ya polisi.
Social Plugin