Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutokwa na machozi akiwa katika ibada katika kanisa la Efatha linaloongozwa na mtumishi wa Mungu Josephat Mwingira kiongozi huyo ameibuka na kutoa neno.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Makonda amechapisha video ambayo alionekana anatokwa na machozi kanisani hapo na kuandika ujumbe ambao alibainisha watu wengi hawajui kilichotokea.
Makonda ameandika; “Powerful, very powerful watu hawaelewi nini kimefanyika Ila mbinguni wameelewa na wameandika, people think it’s a joke. Ila kwa Mungu hakuna mzaha, asante Mungu Kwa kusimama upande wangu”
Hivi karibuni Mkuu wa huyo wa Mkoa Dar es salaam alianzisha kampeni maalum ya kuwakamata watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, na kuunda kamati maalum ya watu 17 ili ya kushughulika na suala hilo.
Jana kupitia ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje, serikali ilisema zoezi linaloendeshwa na Mkonda ni mawazo yake binafsi na si msimamo wa serikali.
Social Plugin