Mbowe ametoa kauli hiyo, akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, baada ya mahakama hiyo kumfutia dhamana na mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko kwa kukiuka masharti ya dhamana hiyo.
Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alitumia kizimba cha mahakama hiyo kusalimiana na viongozi wengine wa Chadema na wafuasi pamoja na kutoa ujumbe wake wa kuwatia moyo.
“Naomba muwe stable (imara), msiogope. Kesho ni nzuri kuliko jana,” alisema Mbowe kisha akamalizia na salamu ya chama hicho ya “peoples” na wafuasi kuitikia “power”.
Kabla ya kutoa ujumbe huo, askari walitaka kumuondoa katika kizimba, lakini akawasihi akisema “kwanza nizungumze na watu wangu”.
Uamuzi wa kuwafutia wawili hao dhamana ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri akisema kitendo kilichofanywa na washtakiwa hao ni kudharau amri za mahakama kwa makusudi.
Social Plugin