Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CUF,ACT,CHADEMA WAUNGANA KESI YA MBOWE,MATIKO


Viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani nchini akiwemo Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe na Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara upande wa Maalim Seif , Joel Luhabara wameonekana kwenye kesi ya dhamana inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Mbali na viongozi hao wakubwa pia mahakamani hapo ilishuhudiwa mamia ya wafuasi wa CHADEMA waliojitokeza kwa ajili ya kusikiliza hatma ya kiongozi wao Freeman Mbowe.

“Tunawaambia wanachama wote kesho saa mbili waje mahakamani, chama chote kitahamia hapa, naomba wanachadema tushikamane kwa ajili ya mwenyekiti wetu.” Amesema Borniface Jacob

Akizungumza nje ya viunga vya mahakama Naibu Katibu Mkuu CUF bara Joel Luhabrua amesema “kwa hali ilivyosasa kuna nguvu ya kutaka kuumiza upinzani, tumeona tuongeze nguvu yetu kwa pamoja, ” Joel Luhabura.

Mbowe na Matiko wamerudishwa rumande kwaajili ya kusubiri kusikilizwa kwa kesi ya kupewa au kutopewa dhamana, Alhamisi ya wiki hii saa mbili asubuhi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com