Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, (kushoto)Meneja Udhamini na Mawasiliano wa TBL,David Tarimo (katikati) na Afisa Kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Humid Semvua wakifuatilia namba ya mshindi wakati wa droo ya kwanza ya mshindi wa gari iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (Kulia) ni Meneja Udhamini na Mawasiliano wa TBL, David Tarimo.
***
Mkazi wa Dar es Salaam na mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Julitha Kilawe, ameibuka mshindi wa gari mpya aina ya Renault KWID kupitia promosheni ya TBL Kumenoga, Tukutane Baa’iliyozinduliwa mwezi uliopita itakayowezesha washiriki 3 wa promosheni hiyo kujishindia gari 1 kila mwezi katika kipindi cha miezi 3 ya promosheni hiyo.
Droo ya kuwapata washindi hao imefanyika jijini Dar e Salaam, chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Taifa na kushuhudiwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Mshindi huyo alipokea habari hizo kwa furaha baada ya kupigiwa na Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, ambapo alieleza kuwa amefurahishwa na kujishindia gari ambalo litamrahishia usafiri katika shughuli zake za kila siku.
“Natoa wito kwa wateja wetu wazidi kujitokeza kushiriki, tumejipanga vyema ili kuwafikia wote nchi nzima. Tumewaletea wateja wetu promosheni hii kwa lengo la kuwashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono”, alisema Tarimo.
Tarimo, aliongeza kuwa, promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa juma yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa muda wa miezi mitatu kupitia bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager. Kwa muda wote huu washiriki wataweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa kabisa ya gari mpya.
Kwa upande wake, Meneja wa Bia chapa ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, alisema mbali na zawadi kubwa ya magari mapya zipo zawadi nyingi za kujishindia papo hapo kwenye promosheni ikiwemo bia za bure, fulana nakadhilika. Alisema promosheni itakuwa inafanyika kwenye mabaa zaidi ya 5000 nchini katika siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. ‘Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga, kwani ilipo bendera hii ndipo wateja na TBL wanapokutana katika promosheni.’
Alisema ili kuingia kwenye droo ya magari mapya ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ wateja watatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni ambapo watapatiwa kuponi yenye namba, kisha watatuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wale wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL. Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya www.tblkumenoga.co.tz.
Social Plugin