Mke wa mwalimu wa Chuo cha Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Manyara, Judith Uromi (32) amekufa kwa kujinyonga na kanga aliyofunga dirishani chumbani kwake kutokana na mgogoro wa muda mrefu wa ndoa.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augustino Senga alisema kilitokea Novemba 10, mwaka huu, saa 1:30 jioni katika maeneo ya Wang’waray karibu na chuo cha Veta wilayani Babati.
Alifafanua kuwa Uromi aliwaaga wanafamilia anaingia chumbani kupumzika saa 12:00 jioni wakati huo mumewe akiwa ametoka na mgeni kwa lengo la kumsindikiza. Hakutoka ndani mpaka alipogundulika amekufa.
Kwa mujibu wake, chanzo cha uamuzi huo wa kujinyonga haujulikani kwani hakuacha ujumbe wowote. Pia alisema Uromi ameacha watoto wawili wa kiume na mwili wake haukuwa na majeraha yoyote.
Chanzo : Habari leo
Social Plugin