MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati akifungua semina ya kodi kwa waandishi wa Habari mkoani Tanga iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Mkoani Tanga (TRA) kushoto ni Meneja wa TRA mkoani Tanga Masawa Masatu
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati akifungua semina ya kodi kwa waandishi wa Habari mkoani Tanga iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Mkoani Tanga (TRA) kushoto ni Meneja wa TRA mkoani Tanga Masawa Masatu na kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (TANGA PRESS CLUB) Hassan Hashim semina hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Bandari Jijini hapa
Meneja wa TRA mkoani Tanga Masawa Masatu akizungumza katika semina hiyo
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (TANGA PRESS CLUB) Hassani Hashim akizungumza katika semina hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA mkaoni Tanga Salim Bakar akizungumza katika semina hiyo kulia ni Meneja wa TRA Mkoani Tanga Masawa Masatu
Mratibu wa Tanga Press Club Neema Omari akiwa kwenye semina hiyo kulia ni Mwandishi wa gazeti la Uhuru mkoani Tanga Sophia Wakati
Makamu Mwenyekiti wa Tanga Press Club Lulu George akifuatilia semina hiyo
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali kwenye semina hiyo
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia semina hiyo katikati ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania na kulia ni Mbaruku Yusuph wa Tanzania Daima
Sehemu ya maafisa wa TRA wakiwa kwenye semina hiyo
Mratibu wa Tanga Press Club Neema Omari kulia akiteta jambo na Mwandishi wa Habari wa TBC Tanga Bertha Mwambela na kushoto ni Sussan Uhinga wa Gazeti la Mtanzania
Mwandishi wa gazeti la Uhuru mkoani Tanga Sophia wakati kushoto akiwa na Mwandishi wa TBC Tanga Joachim Kapembe wakichukua dondoo kwenye semina hiyo
Sehemu ya waandishi wakifuatilia matukio
Mwandishi wa Gazeti la Habari leo mkoani Tanga Cheji Bakari kulia akiwa na Amina Kingazi
Mwandishi wa Habari wa Azam TV mkoani Tanga Mariam Shedafa akiwa kwenye semina hiyo.
****
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka waandishi wa habari mkoani Tanga kusaidia kuwafichua wafanyabiashara wanaopitisha bidhaa kwa njia ya magendo ili waweze kuchukuliwa hatua na kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii badala ya kuendelea kuzikalia.
Mwalipwa aliyasema hayo leo mjini hapa wakati akifungua semina ya kodi kwa waandishi wa habari mkoani Tanga ambapo alisema waandishi wa habari wana mchango mkubwa sana katika suala la kuhakikisha wanapambana kwenye vita ya biashara kwa wanakuwa mstari wa mbele katika kuwatoa taarifa kwa mamlaka husika kuwepo kwa vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.
“Ndugu zangu waandishi wa habari wasidie kuwafichua wafanya biashara wanaopitisha biashara kwa njia ya magendo saidieni kufuichukua hili kwa kutoa taarifa kwa yoyoye anayehusika na uingizaji bidhaa haramu za magendo nawaombeni acheni kuzikalia toeni taarifa kwa mamlaka husika hatua za kisheria zichukuliwe”,alisema Mwilapwa.
Aidha alisema kwamba kwa mwanahabari ambaye atakakuwa ameikalia habari hiyo atakuwa ameitendea dhambi kubwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu atakuwa hajatusaidia katika mapambano ya kuhakikisha tunakomesha tabia hiyo kwenye jamii.
“Lakini pia niwaambie kwamba watu ambao ninaamini wakiingia kwenye vita hii kushirikiana na vyombo mbalimbali watasaidia sana itakuwa wanahabari naombeni sana mshirikiane na serikali kupeana taarifa na kuelimishana lakini pia mtembee na hisia ya serikali kuchukia vitendo hivyo kwani madhara yake ni makubwa kwani vinaikosesha serikali mapato",alisema Mwilapwa
“Pia licha ya mapato lakini Taifa linakosa kitu muhimu ambacho kingekuwa cha manufaa kwa maendeleo yao…kuingiza bidhaa inayopita kwenye milango isiyokuwa rasmi inawezekana bidhaa iliyopita na wakati, feki, lakini pia ni bidhaa duni",alisema.
Awali akizungumza kwenye semina hyo Meneja wa TRA Mkoani Tanga Masawa Masatu alisema kwamba wameamua kuandaa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari ili watambue magendo ni nini na sheria inayosimamia bidhaa zinazoingia nchini inavyoeleza ili watakapotoka wawe mabalozi wazuri kuwaelimisha watu kupitia kwenye milango sahihi kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
“Siku ya leo tumeandaa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari mojawapo ni juu ya masuala ya vita dhidi ya magendo kama TRA tunatambua changamoto ya magendo inayoikabili mkoa wetu na Mkuu wa mkoa ameunda kamati maalumu ya mkoa ambayo itakuwa na jukumu la kukomesha vitendo vya magendo kwa mkoa wetu wa Tanga”,alisema.
“Lakini namshukuru RC kwa kusimamia suala hilo naamini kwamba litakapotekelezwa kwa ukamilifu suala la magendo litapungua kwa asilimia kubwa sana”,alisema Meneja huyo.
Social Plugin