Jaji Mkuu wa shindano ya Bongo Star Search (BSS) Rita Paulsen akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza zawadi na fainali za BSS msimu wa 9 ambapo mshindi atapata zawadi ya fedha taslimu TZS5M pamoja na mkataba wa mwaka mmoja kutoka kwa wadhamini wakuu ambao kampuni ya Mojabet inayojishughulisha na mchezo kupitia Boompesa. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Mojabet Diacha Chacha.
**
KAMPUNI ya Mojabet inayojishughulisha na mchezo wa kubahatisha kupitia mmoja ya michezo yake ya Boompesa leo imetangaza kudhamini fainali za Bongo Star Search (BSS) ambazo zinatarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wakutangaza kudhamini Bongo Star Search msimu wa 9, Mkurugenzi wa Masoko kutoka kampuni ya Mojabet Diana Chacha alisema kuwa wameona ni muhimu kushirikiana na Bongo Star Search ili kuendelea kuimbua vipaji vipya vya muziki hapa nchini na pia kufanya vijana zaidi waweze kujiajiri kupitia muziki.
Sisi lengo ni kuwafanya Watanzania wengi waweze kujiajiri kupitia zawadi za fedha taslimu ambazo huwa tunawapa washindi wetu. Kwa maana hiyo tumeona ni muhimu kutanua wingu wetu na kuelekeza kwenye muziki kwani huko pia kuna vipaji vyingi lakini kutokana na kutopata nafasi ya kuonekana, tunaamini kuwa ushirikiano wetu na BSS utaweza kutanua wingu na kufikia Watanzania wengi na hasa kupitia vijana kupitia Boompesa, alisema Chacha.
Chacha aliongeza kuwa Boompesa ni mchezo ambao unachezwa kwenye mitandao yote ya simu za mkononi kwa kununua tiketi , na mara mshindi anaposhinda anapewa fedha zake papo hapo kwenye simu yake , na mchezaji anaweza kununua tiketi kuanzia shilingi 100 na kuendelea.
Mojabet ni kampuni ya michezo ya Bahati na sibu na Boompesa ni mmoja ya michezo yetu.Mojabet kupitia Boompesa ni wadhamini wakuu katika Bss season 9.na nusu fainali na fainali Boompesa imeandaa zawadi nono na sio kwa washiriki wa bss tu Bali hata kwa wachezaji wa mchezo huo kwa kupitia code ya Bss.kwani kuna TZS 50 milioni imeandaliwa kwa wachezaji.hivyo ni fursa kwa kila MTU kucheza zaidi ili kujiongezea nafasi take ya kushinda.
Kwa upande wake, Mratibu na Jaji Mkuu wa Bongo Star Search Rita Paulsen alisema kuwa fainali za mwaka huu zimekutakuwa tofauti na za miaka iliyopita kwani mshindi mbali na kujipatia fedha taslimu lakini pia ataweza kupata ajira kutoka kwa kampuni ya Mojabet
Mojabet kupitia Boompesa wamefanya fainali za mwaka huu ziwe za kipekee, alisema Rita huku akiongeza kuwa mshindi wa BSS msimu wa tisa atapata fedha taslimu milioni tano, vile vile atakuwa Balozi wa Boompesa kwa muda wa mwaka mmoja ambapo atakuwa analipwa shilingi milioni mbili kwa mwezi.
Tumeingia mkataba wa mwaka na kampuni kubwa ya muziki ambayo itakuwa ikizalishalisha na kusambaza kazi za mshindi wa mwaka huu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Lengo ni kuhakikisha mshindi wetu anakuwa ni staa kweli, alisema Rita huku akitoa shukrani kwa kampuni ya Mojabet kupitia Boompesa kuweza kudhamini mashindano yam waka huu ambayo yamekuwa tofauti na ya miaka ya nyuma.
Vile Vile, Rita aliongeza kuwa wakati wa kilele cha fainali hizo kutachezeshwa mchezo wa Boompesa ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni hamsini.