Picha : RC MONGELLA AFUNGA KIKAO CHA WADAU WA AFYA MKOA WA MWANZA


Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mheshimiwa John Mongella amefunga kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoani Mwanza kilichofanyika kwa muda wa siku mbili Novemba 5 na 6 ,2018 katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.

Kikao hicho kilichofadhiliwa na Asasi ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Initiative (AGPAHI) yenye malengo ya kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia nchini Tanzania,kililenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu afya.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho,Mheshimiwa Mongella amezitaka halmashauri za wilaya kuhusisha wadau wa afya wanapotengeneza bajeti zao ili kuhakikisha miradi mbalimbali inatekelezwa vizuri.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka wadau wa afya mkoani Mwanza kushirikiana na kuhakikisha wanaboresha huduma ya mama na mtoto mkoani humo.

Aidha ameishukuru asasi ya AGPAHI kwa kujitolea kufadhili kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza huku akibainisha kuwa asasi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mheshimiwa John Mongella akifunga kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoani Mwanza kilichofanyika kwa muda wa siku mbili Novemba 5 na 6 ,2018 katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mheshimiwa John Mongella akifunga kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoani Mwanza.
Wadau wa afya wakiwa ukumbini.
Wadau wa afya wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mheshimiwa John Mongella akifunga kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoani Mwanza 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
أحدث أقدم