Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Rehema Chalamila ‘Ray C’ amelitaka Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) likiwa chini ya Waziri Harrison Mwakyembe na Juliana Shonza kumsaidia Muimbaji wa Injili Rose Muhando.
Ray C ametumia ukurasa wake wa Instagram na kusema Rose Muhando ni Mtanzania, anahitaji msaada.
“Wasanii wenzangu na Watanzania kwa ujumla tunamsaidiaje dada yetu….Huyu ni wa kwetu sisi.Naamini kila mtu ana majukumu na shughuli za hapa na pale, lakini huyu dada ni mtanzania mwenzetu, ni dada yetu, ni ndugu yetu, anahangaika tu huko Kenya hana msaada..Waimba injili wote, wasanii wote na watanzania kwa ujumla tunamsaidiaje dada yetu”
“@basata.tanzania@harrisonmwakyembe @juliana_shonza……………..Naamini akipelekwa sehemu anayofaa kuwa atapata msaada,atapona na atasimama tena.Ushuhuda wangu Unatosha kuamini inawekazana.
1.Amepeperusha sana bendera yetu nje ya nchi kupitia muziki wake.
2.Ametupa amani ya moyo miaka na miaka kupitia muziki wake.
3.Ametusaidia sana kiimani kwa nyimbo zake.
4.Tulifarijika pindi tuskiapo nyimbo zake”
“DADA ROSE MHANDO,WEWE NI SHUJAA,NA SHETANI HAPENDI MASHUJAA,PIGANA NALO DADA,PIGANA NALO KIIMANI TU LITASHINDWA DADA.IMANI YAKO TU NDIO ITAKAYOKUSIMAMISHA TENA”
“BADO TUNAKUHITAJI SANA DA ROSE.🇹🇿”
Inaripotiwa kuwa Rose Muhando kwa sasa yupo nchini Kenya akiwa hana msaada na hii ni baada ya video yake kusambaa kwenye Mitandao ya Kijamii akionekana kuombewa.
Social Plugin