Msanii wa Bongofleva Ney Wa Mitego amefungua ukurasa mwingine baada ya kuja na mtindo wa kumwagia maji mashabiki akiwa stejini na mashabiki hao kuonekana wanachanganyikiwa na kushangilia zaidi kitendo kinachohisiwa kuwa ni ushirikishina.
Hata hivyo Nay ameelezea juu ya tuhuma za maji hayo kuwa ya kishirikina na kwamba anateka akili za watu kwa maji hayo na kumshangilia zaidi, ambapo amesema hiyo ni mbinu mojawapo ambayo anaitumia kwa sasa ili kuchangamsha tu watu ambao wanakuwa wanajitokeza kwenye shoo zake.
Nay alielezea zaidi kuwa "jamani mimi si mshirikina sijawahi kujihusisha na masuala ya kishirikina hata siku moja yale maji ni ya kawaida tu ambayo hayana madhara kwa mtu yeyote kwani naweza kumpa hata mtu akayanywa na yasimdhuru, mimi nayatumia tu ili kuwachangamsha mashabiki zangu".
Pia Nay alisema kitendo chake cha kupendwa sana na mashabiki haswa anapokuwa kwenye steji mbalimbali hakuhusiani kabisa na uchawi ila ni kutokana na kwamba nyimbo zake anazoziimba ambazo nyingi ni za jamii na zinagusa maisha halisi ya watu ndo maana amekuwa akipata mashabiki wengi.
Chanzo - EATV
Social Plugin