Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BINTI ANYANYASWA KINGONO UWANJANI...ASHIKWA SHIKWA POLISI WAKITAKA ARUDI NYUMBANI


Muonekano wa Uwanja wa Veltins siku ya mchezo huo Novemba 24, 2018.
Binti ambaye ni shabiki wa mchezo wa soka nchini Ujerumani ameripoti polisi tukio la kunyanyaswa kingono akiwa kwenye uwanja wa Veltins wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani 'Bundesliga' kati ya wenyeji Schalke 04 dhidi ya FC Nürnberg.

Binti huyo mwenye umri wa miaka 22, amesema alikuwa amekaa na mashabiki wa kiume kwenye mchezo ambao ulifanyika Jumamosi iliyopita Novemba 24, ndipo wakaanza kumshika sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwemo kutaka kumvua nguo za ndani.

Ameieleza polisi katika mji wa Gelsenkirchen kuwa alijaribu kuwaambia maafisa wa usalama waliokuwa uwanjani lakini hakupata msaada zaidi ya kuambiwa kuwa kama hapendi aende nyumbani akaangalie mechi kupitia runinga.

Polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ambapo wameweka wazi kuwa katika malalamiko yake, binti amesema alifikia hatua ya kuvuliwa Sidiria na mashabiki hao.

Kwa upande wa klabu ya Schalke 04 nayo imeweka wazi kuwa imeanza uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini mhusika na kuchukua hatua kwa kushirikiana na polisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com