Bw.Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) akimuonyesha eneo Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula itakapojengwa ofisi za Wizara hiyo alipotembelea eneo hilo leo jijini Dodoma.
Mafundi mbalimbali kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) wapo kazini katika eneo la ujenzi wa ofisa za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto.
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula akiangalia ramani ya ujenzi wa ofisi ya wizara yake katika ni Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) na kulia ni wa msimamizi mradi huo Hasani Bendera .
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula akiwa na Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) wakikagua maeneo ya ujenzi wa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifatilia kwa umakini maelezo ya Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula (hayupo pichani) alipotembelea eneo zitakapojengwa ofisa za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto.
Msimamizi mradi huo Bw.Hasani Bendera kutoka shirika la nyumba Tanzania (NHC) akionyesha eneo itakapojengwa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Ardhi nyumba maendeleo ya makazi Mhe.Angelina Mabula alipotembelea eneo hilo leo jijini Dodoma.
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipotembelea eneo zinapojengwa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto leo jijini Dodoma
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula,akimsisitizia jambo Kaimu meneja kutoka shirika la nyumba Tanzania (NHC) kutoka Dodoma kulia ni Frank Mambo,mbunifu majengo wa NHC
Bango likionesha mji wa Serikali ambapo eneo hilo zitajengwa ofisi za wizara mbalimbali Ihumwa jijini Dodoma
Fundi kutoka NHC Yusuph Amir akizungumzia ujenzi wa ofisi ya wizara ya ardhi nyumba maendeleo ya makazi
Picha na Alex Sonna,Fullshangwe blog
Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi imezitaka mamlaka zinazohusika na maji pamoja na umeme kufikisha huduma hizo mapema iwezekanavyo katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma ili kurahisisha ujenzi wa ofisi za Wizara kuanza.
Naibu waziri wa wizara hiyo Angelina Mabula ametoa maagizo hayo leo alipotembelea eneo zinapojengwa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto katika eneo hilo.
Mabula amesema kuwa kutokana na kasi walinayo Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) ambao ndio wanatekeleza ujenzi huo wanaweza kukwamishwa na changamoto ya maji .
“Shirika la Nyumba wako serius kweli na kazi hii maana walipewa kazi ya kujenga ofisi za Wizara tatu baada ya siku mbili tu wakaanza kufanyia kazi agizo hilo, ila changamoto inakuwa kwenye huduma ya maji na umeme ambazo hazipo katika eneo hili.
“Sasa ili kuhakikisha kuwa tunakamilisha ujenzi huu kwa wakati wa siki 30 ni lazima mamlaka husika wahakikishe wanafikisha huduma ya maji na umeme mapema iwezekanavyo, hasa maji ambayo ndio inahitajika katika hatua ya awali,” amesema Mabula.
Aidha Naibu amesema kuwa wakati wanasubiria huduma hiyo kufikishwa wataangalia namna ya kupata maji ya visima lengo ikiwa ni kukamilisha ujenzi huo kwa wakati huku akisema atatembelea tena eneo hilo baada ya wiki moja .
Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo kutoka NHC Hasani Bendera amesema kuw wanatarajia kukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa bila kujali changamoto ambazo zitajitokeza.
“Tusiangalie changamoto, muda tuliopewa si tatizo kwetu kwani tumejipanga kuhakikisha kuwa tunafanya kazi hii kwa wakati, iwe usiku, mchana, kiangazi au mvua ikiwa inayesha, kazi Itafanyika na tutakamilisha kwa wakati,” amesema Bendera
Kuhusu gharama ya mradi huo Bendera amesema kuwa hadi siku ya jumapili Disemba 2, 2018 watapata jibu kamili kuwa mradi huo utagharimu kiasi gani cha fedha.
Naye fundi kutoka NHC Yusuph Amir amesema kuwa kazi ya kusafisha eneo hilo lenye ukubwa wa hekari zaidi ya 20 itafanyika kwa muda wa siku mbili huku akisema kupitia mradi huo Watanzania watapata ajira.
Katika eneo hili ambalo zitajengwa ofisi za Wizara hizo, tayari NHC wapo hatua ya kusafisha huku ujenzi ukitarajiwa kuanza rasmi jumatatu Disemba 3, 2018.
Social Plugin