Bodi ya nyama Tanzania (TMB) imewataka wananchi kula nyama bora na salama kwa kiwango kinachotakiwa ambacho ni wastani wa kilo 50 kwa mtu mmoja kila mwaka.
Hayo yamesemwa na kaimu msajili wa bodi ya nyama Tanzania, Imani Sichazwe leo Jumatano Oktoba 31 wakati akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es salaam.
Sichazwe amesema Tanzania ni nchi ya tatu kwa wingi wa mifugo ikitanguliwa na Ethiopia pamoja na Sudani lakini ulaji nyama umekuwa wa kiwango cha chini chenye wastani wa kilo 15 kwa kila mmoja.
Na Elizabeth Joachim, Mtanzania