Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : PACESHI YAENDESHA MAFUNZO KWA WASAIDIZI WA KISHERIA MSALALA,USHETU NA KAHAMA MJI



Kituo cha Msaada wa Kisheria Shinyanga (Paralegal Aid Center Shinyanga – PACESHI) kwa ufadhili wa Legal Services Facility (LSF) kimeendesha mafunzo kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Ushetu na Kahama kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya kisheria ili kuisaidia jamii.

Mafunzo hayo ya siku tano yameanza leo Jumatatu Novemba 12,2018 na kufunguliwa na Mwenyekiti wa Bodi ya PACESHI,Ziphora Pangani katika ukumbi wa Shinyanga Fairies Hotel mjini Shinyanga.

Akifungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya PACESHI,Ziphora Pangani aliwataka Wasaidizi wa Kisheria kutumia mafunzo hayo kuboresha huduma za sheria kwenye maeneo yao ili wananchi waweze kutambua haki zao.

“Niwapongeze sana mmekuwa mstari wa mbele kutetea haki za wananchi tena bure,naomba kesi zikiwashinda mzilete makao makuu PACESHI lakini pia jengeni mahusiano mazuri na shirikianeni na viongozi wa serikali waliopo katika jamii kwani lengo letu sote ni kuwasaidia wananchi”,alisema Pangani.

Awali akizungumza,Meneja Mradi wa Kuboresha Huduma za Msaada wa Sheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria,John Shija alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kisheria Wasaidizi wa Kisheria wanaotoa huduma za kisheria katika ngazi ya familia,kijiji na kata.

“Tunategemea mwitikio wa kisheria katika maeneo wanayotoka badala ya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuendekeza mila na desturi kandamizi zinazonyima haki wananchi katika masuala mbalimbali ikiwemo mambo ya mirathi,migogoro ya ardhi na ndoa”,alisema Shija.

Alisema wananchi wengi wamekuwa wakikosa haki zao kutokana na kutojua sheria hivyo uwepo wa Wasaidizi wa Kisheria katika jamii ambao wanatambulika katika Mifumo ya Sheria itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapa uelewa wa kisheria wananchi na kuwapa haki wananchi.

“Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa mradi Mradi wa Kuboresha Huduma za Msaada wa Sheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria unaolenga kuwafanya watu wafahamu huduma ya msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria ili wapate huduma bora na stahiki lakini pia kukuza uelewa wa sheria na haki katika jamii”,alieleza Shija.

Aidha alisema mradi huo pia unalenga kuweka mazingira bora ya utoaji wa msaada wa kisheria sambamba na kuweka mazingira endelevu ya utoaji msaada wa kisheria katika halmashauri za wilaya.

Shija alisema katika mwendelezo wa kutoa mafunzo,wanatarajia kuwapa elimu ya sheria Wasaidizi wa Kisheria 110 kutoka halmashauri zote sita za wilaya mkoa wa Shinyanga ambazo ni Ushetu,Msalala,Kahama Mji,Kishapu,Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Msaada wa Kisheria Shinyanga (Paralegal Aid Center Shinyanga – PACESHI),Ziphora Pangani akifungua mafunzo kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Ushetu na Kahama kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya kisheria ili kuisaidia jamii.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Msaada wa Kisheria Shinyanga (Paralegal Aid Center Shinyanga – PACESHI),Ziphora Pangani akifungua mafunzo hayo.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa ukumbini.
Mwenyekiti wa Bodi ya PACESHI ,Ziphora Pangani akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo.Kushoto ni Meneja Mradi wa Kuboresha Huduma za Msaada wa Sheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria,John Shija akifuatiwa na Mwanasheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Lightness Tarimo na Wakili wa Serikali Wizara ya Katiba na Sheria Agnes Tumbuchile.
Wakili wa Serikali Wizara ya Katiba na Sheria Agnes Tumbuchile akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Ushetu na Kahama kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya kisheria ili kuisaidia jamii.
Meneja Mradi wa Kuboresha Huduma za Msaada wa Sheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria,John Shija akielezea malengo ya mafunzo kwa Wasaidizi wa Kisheria.
Meneja Mradi wa Kuboresha Huduma za Msaada wa Sheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria,John Shija akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Meneja Mradi wa Kuboresha Huduma za Msaada wa Sheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria,John Shija akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mwanasheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Lightness Tarimo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Wasaidizi wa kisheria wakiwa ukumbini.
Mafunzo yanaendelea...
Mafunzo yanaendelea..
Mfanyakazi wa PACESHI,Hussein Kiende akizungumza ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Meneja Mradi wa Kuboresha Huduma za Msaada wa Sheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria,John Shija akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Mafunzo yanaendelea.
Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com