Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA RAFIKI SDO LAENDESHA MJADALA WA UKATILI WA KIJINSIA MWAKITOLYO

Shirika la Rafiki Social Development  limeendesha mjadala na kamati ya maendeleo ya kata,viongozi wa dini,wazee mashuhuri ,mjadala wa kupinga na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika kata ya Mwakitolyo,halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga . 


Mratibu wa mradi wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na shirika hilo Charles Ally amesema mradi huo unatekelezwa katika kata nne za halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga(Mwakitolyo,Iselamagazi,Salawe na Lyabukande).

Alisema lengo la mradi huo ni kumaliza kama si kupunguza uwepo wa mimba na ndoa za utotoni. kwa kutoa elimu katika makundi mbalimbali kuanzia ngazi ya familia hadi serikali kumaliza tatizo hilo. 

“Tumekuwa tukifanya mijadala mbalimbali ya kutoa elimu ya haki za mtoto pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia ili kuibadilisha jamii hii inayoishi maeneo ya vijiji kuacha mila,desturi na mambo yanayomkatili mtoto”,alisema Charles. 

“Inawezekana waathiriwa wakawa hawapati msaada sahihi,lakini pia jamii inakuwa na uelewa mdogo kuhusu kuripoti masuala ya ukatili”,alioongez. 

Akizungumza wakati wa mjadala huo afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Opeyo Sisso amesema vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia vinahitaji ushirikiano kuanzia ngazi ya familia,na kuacha uoga wakati wa kesi. 

“Usukumani tatizo la uoga wa kutoa ushahidi na kuficha watuhumiwa kutokana na ujamaa na undugu kunababisha,vita hivi kuonekana vikisuasua kufikia malengo ya jamii salama familia salama” Alisema Sisso. 

Kwa upande wake mwanasheria Senorina Kisunzu amesema sheria ya ndoa imekuwa ikimkandamiza mtoto na kusababisha ukatili wa kingono umetajwa kuwepo katika kijiji cha Mawimilu,kata ya Mwakitolyo na kuwaasa wakaazi kuzigatia mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto.

Tazama picha chini

Afisa mradi wa kupinga ndoa na mimba za utotoni Rafiki SDO Charles Ally akizungumza- picha zote na Malaki Philipo.
Mwanasheria Senorina Kisunzi akifafanua sheria kinzani zinazokandamiza haki za mtoto 
Mjadala ukiendelea
Wajumbe wakifuatilia hoja mbalimbali wakati wa mjadala.
Afisa maendeleo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Opeyo Sisso akiwaeleza wajumbe madhara ya vitendo vya ukatili hasa ngono kwa watoto
Afisa mtendaji wa kijiji cha Mwamamilu Njile Samwel  akieleza mikakati wanayoitumia kumaliza ukatili wa kijinsia.
Mjumbe Kasulu Lubigisa akichangia hoja kwamba Desturi za usukumani zinaruhusu mtoto kuoa ama kuolewa.
Mjumbe Stella Mabula akipinga hoja ya utandawazi kuwa chachu ya ndoa na mimba za utotoni katika maeneo ya vijiji.
Majadiliano yakiendelea.
wanakijiji wa Mawimilu wakisubiri sinema ya ukatili wa kijinsia.
Wakazi wa kata ya Mwakitolyo wakitazama sinema inayohusu vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia,mimba na ndoa za utotoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com