Rais Dkt. John Pombe Magufuli amegoma kuyauzia makampuni Korosho kwa madai kwamba ni wababaishaji na wanataka kuwaibia wananchi.
Badala yake amesema kwamba serikali itanunua korosho yote kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo.
Awali, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kwamba kuna makampuni 13 yamejitokeza kutaka kununua korosho kwa bei elekezi ya tsh. 3000
Aliyataja makampuni hayo kuwa ni Mega movers ambayo inataka tani laki 2, kampuni ya Kitanzania Mkeme Agri inataka tani elfu 5, na makampuni matatu yatachukua tani elfu 5, makampuni manne, tani elfu moja moja.
Ombi hilo limekataliwa na Rais Magufuli kwa madai kwamba wafanyabiashara hao ni wababaishaji, hivyo korosho yote itanunuliwa na serikali kwa sh 3,300 kwa kilo isiyobanguliwa.
“Hawa wanaokuja leo hawa ni ujajnja tuu kwanini hawakuja mwezi uliopita? watakuja Na macondition ya ajabu. Sisi hatuwezi kukaa kimya wakulima wetu wananyanyaswa. TANTrade muanze kutafuta masoko ya mazao mengine kama cocoa Na mengine”. Amesema Rais Magufuli
Social Plugin