Rais John Magufuli amewataka mawaziri kuwa makini na kushirikian ana vyombo vyote kuhakikisha hata korosho moja haipotei.
Aidha, amewataka kufanya maamuzi bila kuamriwa na rais au Waziri Mkuu kwa lengo la kukuza maendeleo ya nchi.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 12, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha mawaziri na naibu waziri aliowateua Jumamosi wiki iliyopita.
“Mawaziri muwe mnafanya maamuzi sio kila kitu Waziri Mkuu au rais wawasaidie kufanya na mimi ninapenda mawaziri wanaofanya maamuzi wenyewe.
“Mnasema mimi mkorofi lakini si kweli ninyi ndiyo wakorofi kwa kuwa hamfanyi yale wananchi wanayotaka mfanye.
“Ni lazima kila mmoja awajibike, mimi sitojali kubaki na mmoja mbona kila siku nabadilisha ni kitu cha kawaida na ninafanya hivyo ili nipate matokeo mazuri, kwanza wabunge wako 365 hata nikiwateua kwa miezi mitano mitano ni sawa tu,” amesema Magufuli.
Social Plugin