Hatimaye msanii wa muziki nchini Rayvann ameamua kuutoa wimbo wake na Diamond Platnumz unaoitwa ‘Mwanza’ baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Wimbo huo wa Mwanza uliopostiwa siku ya Jumamosi kwenye You Tube ulikuwa unashika nafasi ya kwanza kwenye mtandao huo na kufanikiwa kutazamwa na zaidi ya watu milioni 1.9.
Kwa mujibu wa BASATA imewatoza jumla ya milioni tisa, ambapo DiamondPlatnumz milioni tatu, Rayvanny milioni tatu na kampuni ya Wasafi milioni tatu kwa kutoa wimbo usio na maadili ya kitanzania
Social Plugin