Msanii wa muziki Rayvanny amefika kwenye ofisi za Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) baada ya kufungiwa kwa wimbo ‘Mwanza’ kwa madai wimbo huo hauendani na maadili ya Kitanzania.
Rayvany aliwasili katika baraza hilo saa 11:30 akiwa na gari jeupe aina ya Harrier akiwa ameambatana na watu wawili.
Akiwa amevalia suruali nyeusi na sweta la rangi ya machungwa yenye kofia, alijifunika usoni ili kukwepa kamera za wanahabari waliojazana katika ofisi za Baraza hilo zilizopo Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam.
Baada ya kufika hapo aliegesha gari kwa muda kabla ya kuelekea ofisi za Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza.
Social Plugin