Rooney (33) ambaye sasa anakipiga katika klabu ya DC United ya ligi kuu nchini Marekani (MLS) alicheza mchezo wake wa mwisho mwezi Novemba 2016, katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Scotland.
Mchezo huo utakaopigwa Novemba 15 katika uwanja wa Wembley, utakuwa ni mchezo wake wa 120 kwa 'Three Lions' ambapo mpaka sasa ndiye mfungaji bora wa timu hiyo, akifunga jumla ya mabao 53.
Akizungumzia mchezo huo, Wayne Rooney amesema, "ninajisikia faraja kubwa kuheshimiwa namna hii na kuichezea timu ya taifa ya Uingereza. Ninamshukuru Gareth Southgate (kocha mkuu) na FA kwa kunialika katika mchezo huu".
"Yalikuwa ni mafanikio makubwa sana kuichezea Uingereza, kwahiyo kucheza mchezo w 120 itakuwa ni wakati mzuri sana kwangu, pia mchezo wenyewe ni dhidi ya Marekani, kwahiyo mashabiki wangu wa pande zote mbili watafurahi", ameongeza.
Wayne Rooney alijiunga na DC United mwezi Januari mwaka huu akitokea Everton, amefunga jumla ya mabao 12 mpaka sasa na kuitoa klabu hiyo kutoka mkiani mwa ligi hadi kucheza kwenye hatua ya mtoano.
Social Plugin