Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SUGU ACHANA MISTARI BUNGENI ...NGOMA 'ANA MIAKA CHINI YA 18 MBELE YA WAZIRI MKUU


Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ leo ametumbuiza ndani ya ukumbi wa zamani wa Bunge jijini Dodoma, mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika Job Ndugai, Naibu Spika Tulia Ackson na wabunge wengine mbalimbali katika uzinduzi wa Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia ndani ya Bunge.

Sugu alitumbuiza kwa wimbo wake wenye jina Ana Miaka 18 ambao amesema aliutunga zaidi ya miaka 20 iliyopita, baada ya kufanya utafiti na kubaini namna wasichana walivyokuwa wakinyanyasika kijinsia na kubaguliwa hali iliyopelekea pia wakajiingiza katika biashara haramu ya ngono.

Amesema kwa kuwa yeye si msomi, badala ya kupeleka matokeo ya utafiti wake huo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliamua kuwasilisha matokeo hayo kwa njia ya wimbo huo.

Na  Baraka Samson, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com