Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limetoa taarifa kwa klabu zote za ligi kuu Tanzania bara kuwa mechi zote zitakazochezwa katika uwanja wa taifa zitachezwa saa saa 10 jioni.
Taarifa hiyo imekuja kufuatia mmiliki wa uwanja wa taifa kutoa agizo la kutowasha taa katika uwanja huo kwaajili ya mechi za saa 12 na saa 1 usiku kama ilivyokuwa imepangwa katika ratiba ya Bodi ya Ligi.
Utekelezaji wa taarifa hiyo ya wamiliki wa uwanja umeanza mara moja hii leo katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Yanga na JKT Tanzania, mchezo ambao ulikuwa uanze saa 12 jioni.a
Katika ratiba ya Bodi ya Ligi, michezo mikubwa iliyohusisha Simba na Yanga mara nyingi ilipangiwa kuchezwa saa 12 au saa 1 usiku ambapo sasa italazimika kuanza saa 10 jioni
Chanzo:Eatv
Social Plugin