Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwajulisha Wananchi wote kuwa; imefungua Dawati maalumu la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa na kushughulikia maombi yote ya haraka kwa wateja wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wenye hitaji la kufungua Kampuni, Kusajili Nembo za Biashara n.k
Huduma hii ya haraka (Fast Tracking) inatolewa kwenye ofisi zote za NIDA zilipo nchi nzima. Muhimu kuwa na nyaraka za Utambulisho zinazoonyesha hitaji la kufungua Kampuni au kusajili Nembo ya Biashara kulingana na utaratibu utakao elekezwa kwenye kituo chetu.
Kwa wateja ambao hawajaanza taratibu za Usajili wa Vitambulisho vya Taifa mnashauriwa kuanzia Serikali ya Mtaa/Kijiji unakoishi, kujaza fomu ya maombi ya Vitambulisho vya Taifa na kufika kwenye ofisi zetu kwa hatua ya kupiga picha, na kuchuliwa alama za vidole. Muhimu kuzingatia taratibu zote za Usajili na Utambuzi ni lazima zifuatwe kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Usajili.
Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0673 – 333444.
Limetolewa na;
Akital
Dkt. Arnold Kihaule,
MKURUGENZI MKUU
19 NOVEMBA 2018
Social Plugin