Kamishina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Operesheni Kikosi cha Usalma barabarani Makao Makuu ,Abdi Issango,akiongea wakati wa uzinduzi huo,wengine pichani ni Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi (katikati) na Mrakibu wa jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha elimu Tanzania, Abel Swai.
Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa barabara (SUMATRA), Johansen Kahatano ,(Kushoto) akiongea kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ( hawapo pichani) katikati ni Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL Group Irene Mutiganzi na Kamishina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Operaresheni Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu ,Abdi Issango.
Meneja Masuala Endelevu wa TBL Irene Mutiganzi akielezea kampeni hiyo kwa waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa barabara (SUMATRA) Johansen Kahatano, akikabidhiwa Stika kuhusiana na kampeni hiyo na Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL ,Irene Mutiganzi (wa pili kulia) wakati wa uzinduzi Kushoto ni Mrakibu wa jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha elimu Tanzania, Abel Swai na Kamishina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Operesheni Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama barabarani ,Abdi Issango.
Mmoja wa waandishi waliohudhuria uzinduzi huo, Felister Massae akikabidhiwa stika zenye ujumbe wa kuhamasisha Unywaji wa kistaarabu
***
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia yake chapa ya Kilimanjaro imezindua kampuni ya unywaji wa pombe kistaarabu inayojulikana kama ‘Kamata Usukani wa Maisha Yako,Kunywa Kistaarabu.Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam,Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi,alisema katika kufanikisha kampeni hii itakayodumu katika kipindi cha miezi miwili kampuni imeshirikiana na wadau mbalimbali ambao ni Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, SUMATRA, TANROADS na kampuni ya usafirishaji abiria ya UBER.
“Kama kampuni tunajali wateja wetu na pia tunatambua kuwa ni jukumu letu kuelimisha jamii yetu kuhusu madhara ya unywaji pombe kupita kiasi. Elimu hii itatolewa kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari”,alisema Mutiganzi.
Aliongeza kuwa pia itatolewa elimu kwa madereva 150 wa UBER wa mkoa wa Dar es Salaam ili kuwakumbusha kuhusu usalama wao na abiria wao wakati wanapokuwa barabarani na madereva watakaopata mafunzo wataweka stika za ‘Shika Usukani wa Maisha Yako,Kunywa Kistaarabu’ kwenye magari wanayoendesha kama ishara ya kuonyesha ushiriki wao na ahadi yao ya kuzingatia elimu waliopewa.
“Katika siku za karibuni nchi yetu imekumbwa na matukio ya ajali za barabarani na sisi, ndugu zetu, marafiki zetu na wateja wetu tukiwa kama watumiaji wa barabara ni vema kukumbushana jukumu hili la usalama barabarani na kulitafutia ufumbuzi. TBL kwa kushirikiana na wadau wetu tunapenda kuwahamisisha wateja wetu kutokuendesha chombo cha moto pindi wanapokuwa wamelewa na badala yake kutumia usafiri wa UBER au njia nyingine mbadala”,alisisitiza.
Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni kutoka Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdi Issango, alipongeza jitihada hizo zinazolenga kupunguza matukio ya ajali.
“Suala la kupunguza matukio ya ajali nchini hususani za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo vingi na hasara sio jukumu la serikali na jeshi la polisi pekee bali ni jukumu la kila mtanzania,hivyo tunaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha tunafanikisha kupunguza ama kuondoa tatizo hili la ajali hususani zinazotokana na uzembe wa madereva wanaoendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa” alisema Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Abdi Issango.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa usafiri wa barabara kutoka SUMATRA,Bw.Johansen Kahatano alisema, “Kama wadau wa usafirishaji abiria,tunayo furaha kushirikiana na TBL na wadau wengine katika kampeni hii ya kupunguza ajali nchini nasi tutakuwa mstari wa mbele siku zote tutakuwa mstari wa mbele kushiriki katika uhamasishaji wa jamii kuhusu matumizi salama ya vyombo vya usafirishaji ili kukomesha matukio ya ajali hususan zinazotokana na uzembe wa madereva”.
Social Plugin