Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo na Meneja wa Biashara na ukuzaji wa Masoko wa TBL,wakionyesha magari ambayo washindi watajinyakulia kupitia promosheni hii.
-Wateja wahimizwa kuichangamkia promosheni
Mshindi wa kwanza wa gari mpya kupitia promosheni ya ‘TBL Kumenoga, tukutane baa’, kupatikana wiki ijayo kupitia droo ya kwanza itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, amesema tangu promosheni hiyo izinduliwe mapema mwezi huu wateja wengi nchini kote wameendelea kuichangamkia
“Wateja wetu wanaendelea kuchangamkia ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ huku wakijishindia zawadi mbalimbali. Natoa wito kwa wateja wetu wazidi kujitokeza kushiriki, ili kujipatia nafasi ya kuchukua gari mpya. Tumejipanga vyema ili kuwafikia wote nchi nzima. Tumewaletea wateja wetu promosheni hii kwa lengo la kuwashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono na kila mwezi tutakuwa na zawadi ya gari jipya katika kipindi cha miezi 3”, alisema Tarimo.
Aliongeza kusema kuwa promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa wiki yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili nchini kote kupitia chapa za bia za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.
Kwa upande wake, Meneja wa Biashara na ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, alisema mbali na zawadi kubwa ya magari mapya zipo zawadi nyingi za kujishindia papo hapo kwenye promosheni ikiwemo bia za bure. Promosheni inafanyika katika mabaa zaidi ya 5,000 nchini kote. “Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga na promosheni zetu zote kwani ndipo wateja wa TBL wanapokutana na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali na hatimaye kuingia kwenye ndoo kubwa ya magari mapya.
Alisema ili kuingia kwenye droo ya magari mapya ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ wateja wanatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni kisha watapatiwa kuponi yenye namba, watatuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wale wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL. Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya http://www.tblkumenoga.co.tz.
Social Plugin