Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzania (Tanzania Food & Drugs Authority – TFDA) imeendesha mafunzo kwa Wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga ili kuwa
wezesha kujua sheria,kanuni na miongozo inayohusu usindikaji wa chakula salama pamoja na kuongeza kiwango cha uzingatiaji wa kanuni bora za uzalishaji chakula.
wezesha kujua sheria,kanuni na miongozo inayohusu usindikaji wa chakula salama pamoja na kuongeza kiwango cha uzingatiaji wa kanuni bora za uzalishaji chakula.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo Alhamis Novemba 22,2018 yanayofanyika katika ukumbi wa SIDO mjini Shinyanga, yamefunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Akifungua mafunzo hayo,Mboneko alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na changamoto kubwa ya wajasiriamali na wafanyabiashara kutokidhi matakwa ya kisheria yanayosimamiwa na TFDA,TBS na TRA.
“Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wamekuwa wakikiuka sheria kwa kuweka vyakula na vinywaji nje ya maduka,vyakula vinapigwa na jua kila siku halafu bidhaa hizo zinatumiwa na wananchi,hii inahatarisha afya za walaji”,alisema Mboneko.
“Natoa rai kwa uongozi wa TFDA kuendelea kushirikiana na wajasiriamali na wafanyabiashara waaminifu ili wawape taarifa za wajasiriamali na wafanyabiashara wasio waaminifu na kuwachukulia hatua kali za kisheria”,aliongeza Mboneko.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Justin Makisi alisema kutokana na kuwa suala la usafi ni changamoto kubwa inayovikabili viwanda vidogo nchini,mafunzo hayo yatawezesha wasindikaji hao wadogo wa vyakula kujifunza kanuni za usafi ili kutambua mambo ya msingi wanayopaswa kuzingatia kitaalamu.
“Ili kuhakikisha vyakula vinavyosindikwa vinakuwa salama na bora kwa ajili ya kulinda afya za walaji,TFDA imeamua kutoa mafunzo kwa wasindikaji wadogo wa vyakula ambao ukweli ni kwamba bidhaa zao zinasambaa sana, ili kuwapa mbinu za kuwasaidia bidhaa zao zimudu ushindani wa soko na ndani na nje ya nchi”,alisema.
“Tayari tumetoa mafunzo kama haya kwenye mikoa 23,mkoa wa Shinyanga ni wa 24,tunatoa mafunzo haya kwa kushirikiana na TBS na SIDO ikiwa ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo azma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais,Dkt.John Pombe Magufuli ya kuwa na uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025”,alieleza Makisi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifungua mafunzo kwa Wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack leo katika ukumbi wa SIDO mkoa wa Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga.Kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Chakula TFDA,Lazaro Mwambole.Kushoto ni Mwenyekiti wa mafunzo hayo,Juma Nyankanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga.
Wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko.
Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Justin Makisi akielezea lengo la Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzania kuendesha mafunzo kwa wasindikaji wadogo wa chakula ili kuwawezesha kujua sheria,kanuni na miongozo inayohusu usindikaji wa chakula salama pamoja na kuongeza kiwango cha uzingatiaji wa kanuni bora za uzalishaji chakula.Kulia ni Meneja wa TFDA Kanda ya ziwa Moses Mbambe,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko.
Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Justin Makisi akiwataka wasindikaji wadogo wa chakula kufuata sheria,kanuni na miongozo inayohusu usindikaji wa chakula salama.
Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Justin Makisi akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Mkuu Mawasiliano na Elimu kwa umma TFDA Makao Makuu, James Ndege akitaja mada zitakazofundishwa kwa wajasiriamali/wasindikaji wa chakula ambazo ni dhana ya usalama wa chakula,taratibu za kisheria za usajili wa majengo ya kusindika chakula na kutoa vibali vya kusindika chakula,taratibu za kisheria za usajili wa vyakula vilivyofungashwa,ufungaji na vifungashio,uwekaji lebo kwenye vifungashio,teknolojia ya kusindika chakula,taratibu za utoaji alama ya ubora n.k.
Wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Awali Mkaguzi Mkuu wa Chakula TFDA,Lazaro Mwambole akimtambulisha,Meneja wa TFDA Kanda ya ziwa Moses Mbambe (wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Justin Makisi (wa tatu kutoka kushoto).
Mkaguzi Mkuu wa Chakula TFDA,Lazaro Mwambole akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Picha ya pamoja,Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko,maafisa wa TFDA na wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga kundi la kwanza.
Picha ya pamoja,Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko,maafisa wa TFDA na wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga kundi la pili.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin