Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TFF YAFUTA KISHA KURUDISHA TENA RATIBA YA MECHI ZOTE ZA USIKU LIGI KUU TANZANIA BARA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
RELEASE NAMBA 107

RATIBA YA MECHI  ZA USIKU ZA LIGI KUU UWANJA WA TAIFA YARUDISHWA 

Mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizokuwa zichezwe usiku kabla ya kurudishwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam zitaendelea na ratiba ya awali kama inavyoonesha kwenye ratiba.

Baada ya kushauriana/kujadiliana na mmiliki wa Uwanja wa Taifa,changamoto zilizosababisha mechi hizo za saa 12 jioni na saa 1 usiku kurudishwa saa 10 imeshughulikiwa na kumalizwa.

Hivyo mechi zote zilizopo kwenye ratiba ya kuchezwa usiku zitaendelea kama zinavyoonesha kwenye ratiba.


Cliford Mario Ndimbo 
Afisa Habari na Mawasiliano,TFF 
Novemba 30,2018





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com