Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) venye thamani ya milioni 1.5
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) venye thamani ya milioni 1.5
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) vyenye thamani ya milioni 1.5
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi feni kwa ajili ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) juzi ambapo benkio hiyo ilitoa vifaa
vyenye thamani ya milioni 1.5.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi meza kwa ajili ya matumizi ya ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji juzi ambapo benki hiyo ilitoa vifaa vyenye thamani ya milioni 1.5
WAZEE Wastaafu 2000 mkoani Tanga wamenufaika na mikopo kutoka Benki ya Posta (TPB) wenye thamani ya sh.bilioni 6.7 kupitia pensheni zao ambao umeweza kuwasaidia kukidhi mahitaji yao na kuwakwamua kimaendeleo wao na jamii zao.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) zenye thamani ya milioni 1.5.
Vifaa vya ofisi ambavyo vilikabidhiwa ni viti sita, meza moja na feni mbili ambavyo vitawawezesha wazee hao kuweza kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kiofisi hali itakayowasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa ambapo mikopo hiyo bado inaendelea.
Alisema kwamba huo ni mwanzo hivyo wataendelea kushirikiana na wazee wote nchini wa taasisi mbalimbali ili kuweza kuwasaidia kukidhi mahitaji yao hivyo kuwataka wastaafu kuchangamkia fursa hiyo ikiwemo kuwapa elimu namna ya kutumia fedha husika.
“Lakini niwaambie kwamba sisi TPB tunawaambiwa wazee wastaafu nchi nzima tunawajali kwa kutoa mikopo na huduma za kibenki wao wamekuwa wa kwanza kuweza kutoa mikopo kwao kabla ya hapo wastaafu walikuwa wanaonekana kama ni kada ambayo haikopesheni tulianza kutoa mikopo kwa wastaafu kupitia pensheni zao “Alisema.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji aliishukuru benki ya Posta kwa kuwawezesha na kuwathamini kuwapatia vifaa vya ofisi ambavyo vitakuwa chachu ya kutekeleza shughuli zao kwa ufanisi mkubwa.
“Kwa kweli ofisi yetu ilikuwa na changamoto ya thamani hivyo
tulipowaomba TPB hawakusita kutusaidia hivyo tunawaomba tuendelee kuwasaidiana lakini pia niwaombe waliangalie suala la riba kwa wazee",
Alisema wanashukuru sana kutokana na kwamba hapo awali walikuwa hawakopesheki kutokana na kwamba kila mahali walipokuwawakienda walionekana kama hawawezi kupata fedha za mikopo lakini wao waliamua kuwakopesha.
Social Plugin