Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dar es salaam Sophia Mjema akipokea maelezo juu ajali ya treni iliyotokea asubuhi ya leo eneo la Kalakata.
Takribani watu 9 wamejeruhiwa kufuatia ajali ya treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRC) iliyotokea katika eneo la Karakata Ilala jijini Dar es salaam baada ya treni hiyo ya abiria baadhi ya mabehewa yake kuacha njia na kudondoka.
Taarifa ya ajali hiyo ilianza kusambaa kupitia mitandao ya kijamii ambapo ilielezwa treni hiyo ilikuwa ikitokea Pugu, kuelekea makao makuu yaliyopoko Posta kwa ajili ya kuendelea na safari zake za kila siku za kusafirisha abiria.
Kamanda wa Polisi wa Reli Tanzania David Mnyambuga amesema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na kudai jeshi hilo linaendelea kuchunguza.
“Leo saa 12 .45 asubuhi treni hiyo ilipofika maeneo ya karakata Ilala, mabehewa mawili yalidondoka na mengine matatu yalipotea njia iliacha wataalamu wa reli wanaendelea na uchunguzi”, amesema Mnyambuga.
Wakati huo huo Kupitia Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sopghia Mjema alifika eneo la ajali na kuwatembelea baadhi ya majeruhi wa ajli hiyo ambapo amesema "nimefika Hospitali ya Amana kuwapa pole majeruhi wa ajali ya Treni, tuendelee kuwaombea kwa mwenyezi Mungu wapate afueni kwa haraka,hakika wapo katika mikono salama".
Treni hiyo imejibebea umaarufu kama “treni ya Mwakyembe” kufuatia baadhi ya mabehewa kununuliwa wakati Dkt Harrison Mwakyemba akiwa Waziri wa uchukuzi, na kuliongoza shirika hilo la reli Tanzania (TRL) ambalo nalo kwa sasa limebadilika na kuwa Kampuni ya reli ya Tanzania TRC.
Mwanzoni mwa 2015 aliyekuwa Rais wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza kumuhamisha Dk Mwakyembe wizara ya Afrika Mashariki kufuatia mabadiliko ya madogo ya baraza la mawaziri.
Chanzo- EATV
Social Plugin