Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala limesema kati ya waganga wa tiba asili 19,912 waliosajiliwa kote nchini, saba kati yao walikutwa na makosa mbalimbali hivyo kupewa adhabu ikiwemo kufutiwa usajili.
Akizungumza wakati wa kongamano la wanahabari kuhusu tiba asili na mbadala leo Alhamisi Novemba 22, 2018 Msajili wa baraza hilo, Dk Ruth Suza amesema waganga watatu wamefutiwa kabisa usajili na hawaruhusiwi kujihusisha na shughuli hizo.
“Waganga wawili tumewapa adhabu ya kuwasimamisha kwa miezi sita na wengine wawili tumewapatia onyo kali hawa ni wale waganga ambao wamekiuka sheria na kanuni zilizowekwa,” amesema Dk Suza.
Hata hivyo, Dk Suza amesema bado wanaendelea kufuatilia kwa wale waganga wanaotoa huduma bila kusajiliwa na wanawachukulia hatua za kisheria.
Naye Mfamasia wa tiba asili na mbadala, Ndahani Msigwa amesema tangu mwaka 2017 dawa zilizosajiliwa ni 13 na moja ilifutiwa usajili kutokana na kuonekana kuwa haikuwa na ubora uliona kuwa.
“Licha ya baraza kuipa usajili dawa hatuishii hapo tunaanza kuifuatilia na tunaangalia vitu vingi ni lini dawa ilianza kutumika na wagonjwa wangapi aliwahudumia mrejesho kuhusu dawa yake ukoje, hivyo taarifa hizo husababisha dawa usajili,” amesema
Chanzo:Mwananchi
Social Plugin