Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania, imetaja sababu ya kuwakamata na kuwashikilia kwa muda waandishi wa habari kutoka Kamati Maalum ya Kuwatetea waandishi wa habari duniani (CPJ).
Pamoja na kuwaachia huru, idara hiyo imesema inaendelea kushikilia hati zao za kusafiria kwa uchunguzi zaidi.
Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Novemba 8, 2018 Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda amesema, ‘’ni kweli idara yetu iliwakamata waandishi hao katika maeneo ya hoteli waliyofikia na kufanya nao mahojiano, kwa sababu tulifanya uchunguzi na kubaini wanaenda kinyume na masharti yaliyoainishwa katika madhumuni ya ujio wao hapa nchini.”
Mtanda amesema, waandishi hao Angela Quintal na Muthoki Mumo waliingia nchini Oktoba 31, 2018 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar na katika madhumuni ya safari yao walisema wanaingia nchini kwa matembezi ya kawaida na viza yao ilikuwa inafikia ukomo Januari 1, 2019.
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA
Via Mwananchi
Social Plugin