Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BANC ABC YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WATEJA WAKE


Meneja wa Banc ABC Magabe Nyambuche akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
**

Banc ABC katika kuwajali wateja wake wa maeneo mbalimbali
hapa nchini imeanzisha huduma maalumu ya kutumia satellite ili kuwafikia kwa haraka zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha hivi karibuni, Meneja wa Benki hiyo Magabe Nyambuche alisema pamoja na kuboresha huduma za kibenki pia wameanzisha huduma hiyo ya satelite itakayokuwa na uwezo wa kuwafikia hata wateja wa vijijini

Alitaja mikoa ambao kwa sasa wanatoa huduma hiyo ya satellite ni
Arusha,Dar es salaam,Dododma na Mwanza

Alisema kuwa katika msimu huu wa sikukuu ya Chrismas wanatoa
zawadi kwa wateja wote watakao weka pesa kwenye account(fixed account)watapata riba papo kwa papo.


Pia aliwataka wananchi kujiunga na benki hiyo kwa kuwa huduma zake ni nzuri.


Na Pamela Mollel - Arusha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com