Mabingwa watetezi wa michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON), timu ya taifa ya Cameroon unaweza kusema ilijipanga kushiriki michuano hiyo mwaka 2019 bila kuwa mwenyeji.
Taarifa za CAF jana usiku za kuwafutia uenyeji Cameroon zinaweza kuathiri maeneo mengine hususani ya kiuchumi lakini timu yao bado itakuwa na nafasi kwani inaongoza kundi B ikiwa na alama 10.
Pamoja na kuwa Cameroon walikuwa wameshakata tiketi ya kufuzu fainali hizo wakiwa wenyeji lakini hawakuwa wanyonge kwenye kundi lao lenye timu za Morocco inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 8, Comoros yenye alama 5 na Malawi yenye alama 4.
Shirikisho la soka Afrika (CAF), jana lilitangaza kuwa Cameroon imeshindwa kufikia vigezo vya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza mwezi Juni kutoka mwezi Januari.
Kwa mujibu wa Rais wa CAF Ahmed Ahmed amesema nafasi ya kuandaa fainali hizo sasa iko wazi na mwenyeji mpya atatangazwa kabla ya mwisho wa mwaka huu. Cameroon walitwaa ubinga wa AFCON mwaka 2017 nchini Gabon.
Social Plugin