ALIYEHAMIA CCM APATA KIGUGUMIZI KUGOMBEA UBUNGE 2020


Makao Makuu madogo ya CCM Dar es salaam.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Moses Machali, amesita kuzungumzia safari yake ya kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 na kubainisha kuwa hajui kama atawania nafasi yeyote.

Machali amesema hawezi kuzungumzia nafasi ya kurudi bungeni kwa sasa kutokana na kubanwa na taratibu za chama chake ambazo zinamkataza mwananchama wa kawaida kuonesha nia ya kuwania nafasi yeyote wakati kuna viongozi husika.

"Kuhusu suala la kugombea tena ubunge kupitia CCM kwa sasa sina cha kusema, sitaongea kwa sasa kwa sababu nitakuwa nimekiuka misingi ya chama, kwa hiyo nahifadhi maneno yangu," amesema Machali.

"Hata uniulize kwa namna gani, msimamo wangu kugombea nafasi yeyote 2020 bado nitaendelea kutosema chochote, mpaka wakati muafaka utakapowadia" ,ameongeza Machali.

Moses Machali aliteuliwa na Rais Magufuli, Julai 28 mwaka huu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu pamoja na makada wengine waliohama kutoka upinzani na kujiunga na CCM, akiwemo Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi na David Kafulila ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.

Chanzo-EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post