Chama cha Mapinduzi CCM kimewafungulia baadhi ya makada wake waliokuwa ni wenyeviti wa mikoa wa chama hicho ambao walifungiwa kwa tuhuma za kukisaliti chama.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally amesema, "kimepokea maombi ya kufutiwa adhabu ya kufutiwa uanachama, kwa waliokuwa wenyeviti wa mikoa.
Waliosamehewa na kurejeshewa uanachama ni;
1. Ndg. Ramadhani Rashid Madabida (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam).
2. Ndg. Erasto Izengo Kwirasa (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga).
3. Ndg. Christopher Mwita Sanya (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara).
4. Ndg. Salum Kondo Madenge (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni).
Dkt. Bashiru Ally ameeleza pia kuwa Halmashauri Kuu imeazimia kumuweka kwenye uangalizi aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu baada ya kuomba kurudishiwa uanachama kufuatiwa kutuhumiwa kukihujumu chama hicho.
Katika hatua nyingine, kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kimepokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, pia kimepokea na kuridhia kanuni mpya za usimamizi wa fedha wa chama hicho pamoja na kumteua ndugu Abdallah Mtolea kuwa mgombea Ubunge kwenye uchaguzi wa marudio, jimbo la Temeke.
Mtolea alijiuzulu nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo la Temeke na ndani ya Chama cha Wananchi CUF, Novemba 15 katika vikao vya Bunge Jijini Dodoma kwa kile alichokidai kuchoshwa na migogoro ndani ya chama hicho.
Social Plugin