Viongozi wa BAVICHA wakiongozwa na Mwenyekiti Patrick Ole Sosopi walipotinga ofisi ya Jaji Mkuu leo.
Patrick Ole Sosopi amesema wamefikia uamuzi huo kwa kuona hakuna sehemu nyingine wanaweza kupata haki kutokana na viongozi wao wa kitaifa kukosa badhi ya haki ikiwemo kuwaeleza wananchi maendeleo ya kesi zao mahakamani.
''Tumechukua hatua ya kumwandikia barua Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma, kumweleza malalamiko yetu juu ya uonevu wanaofanyiwa viongozi wetu na vyombo vya dola na sasa vimefika mpaka mahakamani sasa ambapo viongozi wetu wana kesi mbalimbali lakini hawapati haki zao'', amesema Sosopi.
Aidha Ole Sosopi, ameongeza kuwa kuna mambo mengi yanayofanyika ambayo yanaenda kinyume na haki katika Mahakama ikiwemo kukamatwa na kupigwa kwa wanachama wa CHADEMA wanapokuwa kwenye majukumu yao ya kichama.
Pia amesisitiza kuwa barua hiyo haiishii kwa Jaji Mkuu pekee bali inakwenda pia kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali Dkt. Adelardus Kilangi pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
Social Plugin