Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amewataja maadui ambao watapelekea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukosa ushindi katika chaguzi mbili zijazo.
Akifungua mkutano wa ndani wa Baraza la uongozi la CHADEMA Kanda ya Pwani, Sumaye amesema kuwa, maadui wa chama hicho ni baadhi ya wanachama wanaoweka maslahi binafsi mbele kuliko ya Chama na ya wananchi waofifisha jitihada za kukijenga.
"Umefika wakati kwa wanachama wetu kufikiria maslahi mapana ya wananchi na chama la sivyo itakuwa vigumu kushika dola, na kama wanachama watajikita kutetea maslahi binafsi kama ilivyotokea kwa baadhi, ni dhahiri lengo la kuongoza nchi halitafikiwa", amesema Sumaye.
Sumaye ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho baadhi ya wabunge, madiwani, wenyeviti wa halmashauri na wanachama wakijiuzulu nafasi zao na kutimkia CCM ambako baadhi yao walipitishwa na kurudi kwenye nyadhifa hizo.
Uchaguzi wa serikali za mitaa nchini unatarajiwa kufanyika mwakani kabla ya uchaguzi mkuu 2020.