Picha : WAFANYAKAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU WASHEREHEKEA SIKU YA FAMILIA KUAGA MWAKA 2018

Wafanyakazi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Acacia kupitia migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na familia zao wamesherehekea siku ya Familia ‘Buzwagi &Bulyanhulu Family Day 2018’ kuaga mwaka 2018 na kukaribisha mwaka 2019.

Sherehe hiyo iliyofanyika leo Jumamosi Disemba 22,2018 katika Viwanja vya Mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama,pia imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ambapo mgeni rasmi alikuwa Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta.

Akifungua sherehe hizo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Bi. Janeth Reuben aliwashukuru wafanyakazi wote wa migodi hiyo kwa juhudi walizofanya katika mwaka 2018 kuhakikisha kampuni ya Acacia inaendesha biashara kwa ufanisi.

“Sote tunatambua jinsi Acacia tulivyopitia katika mazingira magumu sana mwaka huu na uliopita,lakini tumepata faraja kubwa sana kutoka kwenu kwa sababu mmeweza kufikia na kuvuka malengo tuliyojiwekea ikiwemo malengo ya uzalishaji na ya kiusalama,naomba tuendelee na kasi hiyo hiyo mwaka 2019”,alieleza.

“Nawashukuru sana pia wanafamilia waliofika hapa na wale ambao hawakuweza kufika,sisi wafanyakazi hasa wa migodi tunahitaji na tunapata ushirikiano na upendo mkubwa sana kutoka kwa wenzi wetu na watoto kwa sababu mazingira ya kazi yanatulazimu wengi wetu kuwa mbali na familia”,aliongeza Bi. Reuben.

Alisema ushirikiano na upendo wa wanafamilia wakiwemo wenzi na watoto unawatia moyo hivyo kuwawezesha wafanyakazi kufanya kazi kwa amani katika kulijenga taifa la Tanzania.

Kwa upande wake,Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu , Bw. Benedict Busunzu aliwashukuru viongozi mbalimbali wa serikali kwa ushauri na ushirikiano wanaotoa katika kuhakikisha Acacia inaendelea kufanya kazi kwenye mazingira stahiki na kusababisha maendeleo endelevu kwa jamii.

“Licha ya kampuni yetu kupitia katika changamoto za kibiashara,lakini tunajitahidi kadri inavyowezekana kuhakikisha tunaendelea na shughuli za uzalishaji na kwa wakati huo huo kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi wetu”,alisema Busunzu.

Akielezea kuhusu Siku ya Familia yenye kauli mbiu ya ‘Tufanikiwe pamoja’, Busunzu alisema kwa mara ya kwanza mwaka huu Acacia inaadhimisha siku ya familia kwa kukutanisha pamoja migodi miwili ya Buzwagi na Bulyanhulu ili kuimarisha zaidi mahusiano ya kijamii na kiutendaji kazi.

“Hii ni siku maalumu kwa ajili ya kufurahi pamoja na familia zetu na wadau wetu,kupitia siku hii,ninayo matumaini kwamba ushirikiano na mahusiano yetu na familia na wadau wetu yataimarika ili kutengeneza kesho iliyo bora zaidi kwa sisi sote”,aliongeza Busunzu.

Maadhimisho ya Siku ya Familia Buzwagi na Bulyanhulu yameongozwa na shughuli mbalimbali ikiwemo wanafamilia kutembelea mgodi wa Buzwagi,uchangiaji damu,maonesho ya kazi za wadau wa Acacia,michezo na burudani kadha wa kadha zikiongozwa na Wasanii Banana Zoro na Barnaba.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog ,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri...Tazama hapa chini
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben akifungua sherehe za Siku ya Familia ya Buzwagi na Bulyanhulu niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta leo Disemba 22,2018 katika viwanja vya Mgodi wa Buzwagi uliopo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu , Bw. Benedict Busunzu akielezea kuhusu Siku ya Familia ya Acacia mwaka 2018. Alisema kwa mara ya kwanza wameamua kuadhimisha siku ya Familia kwa kuwaleta pamoja wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na familia zao ili kuimarisha ushirikiano zaidi.
Wanafamilia kutoka kwa wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiangalia eneo la wazi la uchimbaji madini katika mgodi wa Buzwagi.
Muonekano wa eneo ambapo madini ya dhahabu huchimbwa katika mgodi wa Buzwagi.
Wanafamilia wakiangalia mgodi wa Buzwagi.
Wanafamilia wakiangalia eneo la uchimbaji madini katika mgodi wa Buzwagi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Familia Buzwagi na Bulyanhulu, Kambula Lumbu akitambulisha wajumbe waliofanikisha maadhimisho ya sherehe hiyo.
Wanafamilia wa Buzwagi na Bulyanhulu wakicheza muziki.
Kiongozi wa Usalama na afya katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, Dk. Antonette George akimtangaza Hermangild Seki kutoka mgodi wa Bulyanhulu na Elizabeth Sambuka kutoka mgodi wa Buzwagi kuwa ndiyo wafanyakazi bora mwaka 2018 kutokana na kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha usalama mgodini.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta akimkabidhi cheti cha pongezi Hermangild Seki kutoka mgodi wa Bulyanhulu (kushoto).Katikati ni Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, wa kwanza kulia ni Meneja Uboreshaji Tija migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ,Shukuru Mwainunu. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Mgodi wa Buzwagi, Blandina Munghezi.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta akimkabidhi cheti cha pongezi Elizabeth Sambuka kutoka mgodi wa Buzwagi. Katikati ni Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, wa kwanza kulia ni Meneja Uboreshaji Tija migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ,Shukuru Mwainunu.
Hermangild Seki kutoka mgodi wa Bulyanhulu na mkewe wakipokea zawadi ya majiko ikiwa ni zawadi ya ushindi iliyotokana na kuwa mstari wa mbele kuimarisha usalama mgodini.
Elizabeth Sambuka kutoka mgodi wa Buzwagi akipokea zawadi ya majiko ya kupikia.
Picha ya pamoja,viongozi wa Acacia na wafanyakazi bora mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu na familia zao.
Watoto wa wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu picha ya pamoja na viongozi wa Acacia kabla ya kukabidhiwa zawadi.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia akikabidhi zawadi ya madaftari na kalamu kwa watoto wa wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Msanii Banana Zoro akitoa burudani wakati wa sherehe za Siku ya Familia Buzwagi na Bulyanhulu,
Banana Zoro akiendelea kutoa burudani kupitia B Band.
Ashura Mahenge kutoka B Band akiimba nyimbo Live.
Msanii Barnaba akiimba na kucheza na watoto wa wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Msanii Barnaba akigawa zawadi ya pipi kwa watoto.
Wanafamilia wakifuatilia burudani.
Wanafamilia wakiwa eneo la tukio.
Wanafamilia wakiwa eneo la sherehe.

Watoto wakiendelea na michezo yao.
Watoto wakiendelea kucheza.
Watoto wanaendelea kucheza.

Watoto wakipewa zawadi ya vitafunwa.
Watoto wakiendelea kupewa zawadi.
Wafanyakazi wa Acacia wakipiga picha ya kumbukumbu.
Wafanyakazi wa Acacia na familia zao wakiwa katika viwanja vya mgodi wa Buzwagi kushuhudia michezo mbalimbali.
Mchezo wa kukimbiza kuku ukiendelea
Mtoto akiwa na kuku wake baada ya kufanikiwa kumkamata.
Wanafamilia wakiangalia michezo iliyokuwa inaendelea.
Mchezo wa kubeba wenza ukiendelea...kila mmoja kabeba mke wake.
Washindi wa shindano la kubeba wenza wakinyoosha mikono kuonesha wamekuwa wangapi... walipewa zawadi ya Shampen.
Mbio za magunia nazo zilikuwepo.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia akimpa zawadi mshindi wa mbio za magunia, Imani Abdalah.
Wanafamilia wanaangalia michezo iliyokuwa inaendelea.
Mchezo wa kuvuta kamba pia ulikuwepo...hapa wanajiandaa kuvuta kamba.
Washiriki wakijiandaa kuvuta kamba.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia akishikana mkono na Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu , Bw. Benedict Busunzu ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu 'Basket ball' kabla ya mechi kuanza. 
Mpira wa kikapu ukiendelea.
Wanafamilia wa Acacia wakiangalia mpira wa kikapu.
Wafanyakazi wa Acacia wakiwa eneo la tukio.
Wanafamilia wakipata huduma ya chakula.
Wanafamilia wakiwa eneo la tukio.
Sherehe inaendelea.
Sherehe inaendelea
Wanafamilia wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia,akikagua mabanda wakati wa sherehe za Siku ya Familia Buzwagi na Bulyanhulu. Hapa ni katika banda la Acacia akipata maelezo kutoka kwa Mwandindi Charles namna wanavyofanya shughuli za uchimbaji katika mgodi wa Buzwagi.
Andrewe Milambo akionesha mchoro kuhusu shughuli za uchimbaji madini katika mgodi wa Bulyanhulu.
Mchoro kuhusu shughuli za uchimbaji madini katika mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja wa NHIF mkoa wa Shinyanga Imani Emmanuel akitoa maelezo kuhusu bima za afya.
Hapa ni katika banda la Jubilee Insurance life.
Hapa ni katika banda la benki ya NMB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Janeth Reuben akiangalia mafuta ya kupaka yaliyotengenezwa kwa asali na kikundi cha wajasiriamali wa Mwendakulima waliowezeshwa na Acacia.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Janeth Reuben  akinunua batiki iliyotengenezwa na wajasiriamali waliowezeshwa na Acacia.
Wajasiriamali waliowezeshwa na Acacia wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye banda lao la maonesho.
Mtaalamu wa Mawasiliano Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu,Mary Lupamba na mmewe na mtoto wao mchanga wakipiga picha ya kumbukumbu.
Wafanyakazi wa Acacia wakipiga picha ya kumbukumbu.
Ma DJ waliofanikisha sherehe ya Familia ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiwa katika pozi.
Burudani kutoka B Band ikiendelea.
Msanii Banana Zoro kutoka B Band akicheza na wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post