Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA nchini imekanusha taarifa ya kuzuiwa kwa ndege za Shirika la Ndege la Fastjet, kama ilivyoelezwa na Mwenyekiti Mtendaji wa shirika hilo Laurence Masha, kwa kile ilichokisema ilipokea barua ya shirika hilo Desemba 24 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema baadhi ya barua za kuomba kuwasilisha ndege hizo zilifikishwa kwao Desemba 24 na hazikushughulikiwa kutokana na kuwa ni kipindi cha sikukuu.
"Nakanusha taarifa si za kweli hatujawahi kukataa ombi la kuleta ndege na hatuwezi kukataa kwa sababu ni maagizo tuliyowaambia." amesema Johari.
"Walileta andiko la mabadiliko ya utawala na fedha tarehe 24 Desemba mwaka huu , na wataalamu wameanza kulifanyia kazi na muda si mrefu tutawajibu," ameongeza.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema miongoni mwa masharti ambayo shirika hilo halijafanyiwa kazi ni upatikanaji wa mtaalamu wa uendeshaji wa masuala ya ndege ikiwa ni takwa la kisheria.
"Tuliwaambia wateue 'Accountable Manager' lakini siku ya Desemba 24, tulipokea barua kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Fastjet ambaye ni Laurence Masha, amejiteua mwenyewe kuwa mtaalamu wa ndege wa Fastjet." amesema Johari.
Desemba 17 mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania ilitangaza kutoa siku 28 kwa shirika la ndege la Fastjet kushughulikia baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo kulipa madeni wanayodaiwa.
Hapo chini kuna nukuu ya mambo aliyoyasema.
1.FastJet hawakuwa na ndege hata moja hivyo kama mamlaka ya TCAA hatuna budi kuwazuia, wanamadeni ya 6 billion japo wamelipa kidogo, lakini sheria inawataka walipe yote, hivyo kama wao wanahitaji kufanya biashara wafuate masharti na walipe madeni.
2.Tulipata taarifa kupitia vyombo vya habari kwamba tarehe 22 Disemba 2018 wangeleta hizo ndege zao, lakini mamlaka haikuwa na taarifa hizo na wao utaratibu wa kuingiza ndege nchini wanaujua.
3.Ilipofika Tarehe 24 Disemba 2018 saa 6 mchana ndo wakatuma email ya maombi ya kuleta ndege hizo zenye usajili wa Afrika Kusin.
4.Ikumbukwe kwamba, tarehe 25 ilikuwa ni sikukuu na tarehe 26 ilikuwa ni Boxing Day hivyo sote hatukuwa ofisini. Wanaposema et tumewazuia kuzileta ni waongo.
5.Katika notisi ya siku 28 tuliyowapa, tuliwataka Fastjet walete andiko la kudhibitisha uwezo wa kufedha ili kuona kama wanajiweza na pia walete Meneja Mwajibikaji mwenye utaalamu na mambo ya ndege. Fastjet hawakuletea hivyo vitu
6.Badala yake Tar 24.12.2018 ndo sasa wakaleta maombi na barua ya mkurugenzi mtendaji wa Fastjet Lawrence Masha wakitujulisha kuwaLawarence Masha amejiteua mwenyewe kuwa accountable manager.
7.Fastjet waache mzaha. FastJet itakufa kwasababu zao wenyewe maana wanamatatizo mengi, TCAA tunasimamia sheria ili kulinda usalama wa abiria, kulinda maslahi ya watoa huduma (supplies). Habari zote zilizoelezwa si za kweli ni upotoshaji mtupu.
Social Plugin