Mwanaume mmoja amenusurika kifo baada ya kumwagikiwa na grisi na kushindwa kutembea siku mbili
Mwanaume huyo ameokolewa baada ya kukwama katika tanuri la grisi katika mgahawa wa chakula cha wachina katika mji wa Califonia, polisi wamesema.
Kikosi cha dharura kiliitika mwito wa mwanaume huyo aliyekuwa taabani akiomba msaada kutoka katika jengo lililokuwa eneo la San Francisco.
Mwanaume huyo alidai kuwa bado anajisikia uchovu na kuishiwa nguvu lakini anatarajia kuwa atapona kabisa.
Polisi wanasema kwamba inawezekana alikuwa anapita njia ambayo hairuhusiwi kupita lakini hawajaweka wazi kama tukio hilo lilikuwa ni jaribio la wizi au la.
Polisi na kikosi cha zima moto walifika katika eneo la tukio huko San Lorenzo lililopo karibu na Oakland majira ya saa tatu na nusu (17:30 GMT) na sauti ya mtu huyo ilisikika ikiwa inatoka juu ya paa kwenye tanuru linalomilikiwa na mgahawa.
Iliwabidi wapande ngazi ili kufika katika eneo hilo ambalo kijana mwenye umri wa miaka 29 alikuwa ameganda huku akiwa na grisi pamoja na mafuta mwili mzima.
Iliwachukua saa zima kumtoa mwanaume huyo ambaye walimpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu.
Watu wa huduma ya dharura walisikia sauti yake kutoka juu ya paa ya mgahawa
Uchunguzi bado unaendelea kubaini kama mwanaume huyo alikuwa ana nia ya kutaka kuiba au hapana.
Waliongeza kwa kuwashukuru sana kikosi cha wazima moto kwa kumuokoa mtu huyo ambaye asingeweza kupona kama angeendelea kukaa hapo siku nyigine.
Chanzo- BBC