SERIKALI KUTUMIA MUZIKI WA HIPHOP KUJINADI


Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kusini mwa Tanzania Mbeya ,SELEMENTALLY ameiomba serikali kutumia muziki wa Hiphop kwenye kampeni zake za maendeleo kwa kuwa muziki huo licha tu ya kuburudisha umekuwa ukielimisha kwa kiasi kikubwa.

Akiongea na malunde blog kwa njia ya mtandao Selementally amesema kuwa muziki wa Hiphop unauwezo wa kubeba ujumbe na kufikisha kwenye jamii na ukapokelewa kwa mtazamo chanya tofauti na miziki mingine.

“muziki wa Hiphop unaongelea maisha halisi kabisa ya watu huko mtaani ,kama utatumiwa kwenye kampeni mbalimbali za maendeleo unaweza ukabadilisha na kuleta matokeo chanya ni nyimbo zinazoweza kubadilisha fikra za watu” alisema Selementally

Katika hatua nyingine Selementally amewakumbusha waasanii wenzake kuacha kutunga mashairi ya kusifia starehe pekee waikumbuke na jamii,kama alivyofanya Prof. Jay kupitia wimbo wake wa ndio mzee pamoja na Darasa na sikati tamaa.

“wasanii wenzangu wa hiphop baada ya kuimba bata (starehe), pia tukumbuke kuimba vitu vya msingi tuifanye jamii yetu iwe smart”

Hivi karibuni Selementally aliachia video ya wimbo wake unaoitwa anaunguruma akimshirikisha Recho wimbo huo unazungumzia kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

angalia hapa chini



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post