Picha : HUYU NDIYO MISS WORLD MWAKA 2018..ANATOKA MEXICO

Miss world 2018 Vanessa Ponce De Leon

Mrembo kutoka Mexico, Vanessa Ponce De Leon, ameshinda taji la urembo wa Dunia 2018 Sanya, China.

Wakati Vanessa akishinda taji la Dunia 2018 mrembo kutoka Uganga, Quiin Abenakyo, ameiwakilisha vyema Africa mashariki, kwa kutwaa taji la mrembo wa Dunia Africa.

Mrembo kutoka Tanzania, Queen Elizabeth Makune, licha ya kuchuana vikali na Mrembo kutoka Uganda, katika kipengele cha Kura hajabahatika kuingia hata 30 bora kwenye mashindano hayo.

Abenakyo, amefanikiwa kuingia kwenye 30 bora na baadae kuingia katika hatua iliyofuata ya 12 bora na kuendelea kupiga hatua kubwa zaidi mpaka kufika tano bora.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم