Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

IGP AFANYA MABADILIKO JESHI LA POLISI...AMTEUA AHMED MSANGI KUWA MSEMAJI WA POLISI


Mkuu wa Jeshi la Polisi chini, IGP Simon Sirro.

Mkuu wa Jeshi la Polisi chini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko katika jeshi hilo na kuwabadili baadhi ya makamanda vyao vya kazi akiwemo RPC wa Mtwara Lucas Mkondya.

Akizungumza na wanahabari leo, jijini Dar es salaam, aliyekuwa Kamanda wa Polisi jijini Mwanza, Ahmed Msangi ambaye sasa amekuwa Mkuu wa kitengo cha Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Polisi akichukua nafasi ya Msemaji wa Polisi, Barnabas Mwakalukwa, amesema mabadiliko hayo ni ya kawaida.

Kamanda Msangi amesema kuwa, "Aliyekuwa Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Barnabas Mwakalukwa, anakwenda kuwa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Pwani huku aliyekuwa mnadhimu wa Pwani sasa anakwenda kuwa RPC wa mkoa wa Mtwara akichukua nafasi ya Lucas Mkondya aliyehamishiwa kitengo cha Intelijensia ya Makosa ya Jinai Makao Makuu Dar es salaam".

Katika hatua nyingine, Kamanda Msangi amewatahadharisha waganga wa kienyeji wanaotumia ramli chonganishi kuacha mara moja kwa kua tayari makamanda wote wa jeshi hilo hapa nchini wameshapewa maelekezo kuhusiana na watu hao ambao wanakwenda kinyume cha sheria na taratibu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com